Mahali pa Kiswahili Lugha nyinginezo

Sinema Ya YESU

Yamkini umeona sinema nyingi lakini sinema ya Yesu ni ya tofauti. Ni wasilisho la moja kwa moja la maisha ya YESU na kikawaida linabadilisha maisha.

YESU ni sinema ilitotafsiriwa kwa lugha nyingi kuliko sinema ingine katika historia. Sababu yake ya kufuzu ulimwenguni kote na kuvutia watu ni ukweli yake; jinsi inavyo ambatana na vile kulivyotendeka na jinsi ilivyoiga kila kitu kwa makini sana.

Injili kama alivyoandika Luka katika Biblia Takatifu ilichaguliwa kama asili ya mazungumzo na pia uigaji kwenye sinema hii. Miaka mitano ya utafiti ya makini na matayarisho yalifanywa kabla picha za sinema hii hazijachukuliwa huko nchini mwa Israeli. Wanatafiti mbalimbali, wanahistoria na wanatheologia walishauriwa. Mitambo maalumu ilitengeneza vyungu, vifaa na nguo kama zile zilizotumika Karne ya kwanza.

"Kuchagua waigizaji kuiga maisha ya wakati wa Yesu ilifanywa kwa makini sana, haswa yule aliyechaguliwa kuiga Yesu. Kupata nyuso zilizofaa, waigizaji 45 walioonyeshwa sana kuliko wengine, na wengine zaidi ya 5,000 wote walichaguliwa kutoka watu walioishi sehemu ya ulimwengu ya Mashariki ya Kati. Brian Deacon, kutoka kampuni ya Royal Shakespeare huko Uingereza, ndiye aliyechaguliwa kuigiza Yesu. Deacon alichaguliwa kutoka kikundi cha watu 1000 kwa sababu ya jinsi alivyoigiza vizuri hadithi ya Yesu kama vile ilivyoandikwa katika Injili na Luka Mtakatifu."

Hadi wa leo, sinema ya YESU imetafsiriwa hadi lugha zaidi ya 723. Watu zaidi ya bilioni 4 wameiona kote ulimwenguni. Sinema hii ilidhaminiwa na Campus Crusade for Christ International. Upigaji wa picha uliongozwa na John Heymann, mshindi wa zawadi katika Cannes Film Festival. Kampuni ya Warner Brothers ndiyo iliyosimamia kutolewa kwa picha hii kwa mara ya kwanza huko Kaskazini ya Marikani.

Nyumbani Yesu ni nani? Sinema Ya  YESU Kanuni Nne za Kiroho Maisha Yaliyojaa Roho Mtakatifu Fursa Zana

© 1995-2003 Campus Crusade for Christ International

Last Updated: 28 May, 2002